SHULE YA SEKONDARI KIBAHA YAIBUKA YA KWANZA KITAIFA KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA KWA MWAKA 2018

The News Image

SHULE YA SEKONDARI KIBAHA YAIBUKA YA KWANZA KITAIFA KATIKA MITIHANI YA KIDATO CHA SITA KWA MWAKA 2018

Tarehe 13/07/2018

Shule ya Sekondari Kibaha yaibuka ya kwanza kitaifa  katika mitihani ya kidato cha sita kwa mwaka 2018. Matokeo hayo yametangazwa rasmi na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibaha Bw.Chrisdom kwa Ambilikile mbele ya wanafunzi waliokuwa wamemekusanyika katika eneo la mikutano la Shule ya Sekondari Kibaha baada ya matokeo hayo kutangazwa rasmi na NECTA.

Bw. Ambilikile amesema Shule yake imekuwa ya 1 kati ya shule 543 za Sekondari zilizofanya Mitihani ya Kidato cha sita mwaka 2018 . Pia amesema  kwa kawaida Shule yake imekuwa ikifanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ila mwaka huu hii ni mara ya kwanza kuwa ya kwanza kitaifa. Amewapongeza wanafunzi wote waliofaulu mitihani hiyo huku akiwapa pongezi lukuki walimu wa Shule hiyo kwani walijitoa mchana na usiku kuhakikisha wanafunzi hao wanafaulu mitihani hiyo.

Naye Mwalimu wa Taaluma wa Shule hiyo Mwalimu Jonas Mtangi amewaeleza wanafunzi kuwa wanatakiwa waendeelee kujisomea kwa bidii ili kuweza kushikilia taji la mafanikio  yaliyopatikana.

Matokeo hayo yanaonesha kuwa Mwanafunzi Bora kitaifa pia ametoka katika Shule ya Sekondari Kibaha ambaye ni Elihuruma Ngorope aliyeshika nafasi ya kwanza kitaifa kupitia masomo ya Biashara. Matokeo kwa ujumla yanaonesha kuwa wanafunzi 101 wamepata daraja la kwanza,17 daraja la pili na wanafunzi 3 wamepata daraja la tatu.